Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini mchana wa jana, Jumapili, Agosti 30, 2009, kwenda Tripoli, kuhudhuria Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
Katika mkutano wao uliopita wa Juni, mwaka huu, viongozi hao wa AU walikubaliana kuitisha kikao hicho maalum kujadili kwa kina migogoro ya Bara la Afrika na kuitafutia majawabu.
Mbali ya kuhudhuria mkutano huo maalum, viongozi hao wa Afrika watashiriki katika sherehe kubwa za kuadhimisha miaka 40 ya Mapinduzi ya Libya.
Sherehe hizo za kuadhimisha Mapinduzi ya Al Fateh Revolution ama First September Revolution, ni kumbukumbu za siku ambayo Gaddafi alikamata madaraka ya kuitawala Libya kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi usiku wa kuamkia Septemba Mosi, mwaka 1969
Monday, August 31, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment