Thursday, February 11, 2010

Maadhimisho Miaka 20 tangu kuachiwa huru.


Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa kijiji kidogo cha Mvezo wilaya ya UMTATA katika mji uitwao Transkei maana ya neno hilo ni (the area beyond the river) eneo pembezoni mwa mto,nchini afrika kusini tarehe 18 mwezi wa 7 mwaka 1918. Baba yake mzazi alimpa jina la ( ROLIHLAHLA ) maana yake ni parua matawi kwenye mti kwa ufasaha zaidi MSUMBUFU au MKOROFI. Jina hilo hakupewa mpaka alipoanza siku ya kwanza kwenda shuleni. Baba yake mzazi alikuwa chifu Henry Mandela kutoka kabila la Tembu. Nelson Rolihlahla Mandela ni mtoto wa mke wa tatu,NOQAPHI NOSEKENI. Mandela ni mtoto wa 13 wa chifu huyo. Mama yake Mandela alikuwa mmumini wa dhehebu la methodisti,Mandela amefuata hatua za mama yake kwa kujiunga na shule ya waumini wa methodisti.

Mandela alipata elimu katika chuo cha Fort Hare na Witwatersrand na kuhitimu shahada yake ya kwanza 1942 na hapo ndipo alipokutana na rafiki yake Oliver Tambo . Mwaka 1944 alijiunga na chama cha siasa nchini humo African National Congress na kujikita kupambana na chama tawala yenye sera za kibaguzi baada ya mwaka 1948 alishtakiwa kwa makosa ya uhaini 1956-1961 na kuachiwa mwaka 1961.

Mwaka 1940 alifukuzwa na rafiki yake Oliver Tambo kutoka Fort Hare kutokana na kujihusisha na masuala ya kiasa na baada ya kurudi Transkei,Mandela akagundua ndugu zake wameshamwaandalia mipango yake ya harusi baada ya kubaini akaelekea Johannesburg, baada ya kufika huko akapata kazi kama mlinzi wa machimbo ya dhahabu.

Mandela akaanza kazi kama karani katika ofisi za wanasheria,na kusoma masomo ya jioni katika chuo kikuu cha afrika kusini ( University of south Africa ) kwasasa kinaitwa UNISA na kuhitimu shahada yake ya kwanza mwaka 1941 na mwaka 1942 akaanza kufanya kazi katika ofisi ya mawakili na baada ya hapo akaanza kusomea shahada ya sheria katika chu cha kikuu cha Witwatersrand huku akiendelea na masomo yake akakutana na swahiba wake SETSE KHAMA , baadae akawa Rais wa kwanza wa Botswana kuchaguliwa.

Mwaka 1948 Mandela alifeli mtihani wa sheria ambayo ingemruhusu kufanya shughuli za wakili.

1951 Mandela akawa Rais wa chama cha siasa cha umoja wa vijana wa African National Congress.

5 desemba 1956 serikali ya ubaguzi ya afrika kusini iliwakamata jumla ya watu 156 pamoja na Rais wa chama cha siasa cha African National Congress Chifu Albert Luthuli na Nelson Mandela.

Mandela alifungwa gerezani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 1964 mwezi wa 6 na kuachiwa mwaka 1990 februari 11 katika vifungo chake chote alikuiwa katika gereza la Robben Island. Mzee Mandiba ameshapokea tuzo zaidi ya 250 kwa zaidi ya miongo minne na mwaka 1993 alipata tuzo ya AMANI ya NOBEL na mwaka jana mwezi wa Novemba baraza la Umoja wa Mataifa watakuwa waadhimisha siku ya kuzaliwa ya Mzee Mandiba Tar 18 Julai kila mwaka kuanzia mwaka jana kutokana na mchango wake duniani kudumisha Amani.

Huyo ndiye Mzee Mandiba,Nelson Mandela na siku hii ya leo ni kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu aachiwe huru kutoka gerezani…………….

No comments: