Kutokana na misukosuko ambayo imemkumba mcheza gofu namba moja duniani TIGER WOODS mke wake ELLIN inasemekana ameamua kutengana na mwanagofu huyo katika sherehe za mwaka mpya.
Mmoja wa marafiki wa ELLIN amekiambia kituo kimoja cha televisheni nchini MAREKANI kuwa mwanadada huyo yuko imara na hapendi kuaibishwa na anahitaji muida wa kufikiria zaidi watoto wake na kuna habari kuwa hata pete ya ndoa haipo mkononi huku akiwa tayari ameshakutana na mwanasheria kujadiliana jinsi ya kutalikiana na mumewe..
Kwa upande mwingine nyota ya mwanagofu huyo TIGER WOODS imezidi kung’ara baada ya hapo jana kuibuka mwanamichezo mwongo mmoja kwa kupata kura 56 kati ya 142 zilizopigwa na wanachama cha shirika la habari la marekani ambao ni wahariri wa habari za michezo.
Aliyechua nafasi ya pili ni LANCE ARMSTRONG ambaye ni mwendesha baiskeli aliyepata kura 33, watatu ni mcheza tenesi ROGER FEDER aliyepata kura 25,
MICHAEL Phelps kura 13, na tom brady kura 6 huku mwanariadha mwenye kasi kuliko wote duniani USAIN BOLT akiambulia kura 4 tu.
Thursday, December 17, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment