Saturday, November 28, 2009
Mbegu za Kiume za Beckham Euro Milioni 75
Wanawake matajiri wanaotaka watoto wanaofanana na watu maarufu duniani wameongezeka kwa wingi na kuifanya benki ya mbegu za kiume yenye makazi yake California nchini Marekani Cryobank ijaribu kununua mbegu za kiume za watu maarufu.
Cryobank inadaiwa kumfuata mchezaji nyota wa Uingereza anayesakata kabumbu nchini Marekani, David Beckham na kumshawishi awauzie mbegu zake za kiume kwa euro milioni 75.
Hata hivyo inadaiwa kuwa David Beckham alikataa dili hilo.
Cryobank mbali ya Beckham inadaiwa kuwafuata pia nyota kibao wa filamu wa nchini Marekani wakiwataka wachangie mbegu zao za kiume kwenye benki hiyo kwa malipo ya mamilioni ya Euro.
Mmoja wa nyota hao ni Brad Pitt aliyeambiwa atalipwa euro milioni 60 iwapo atachangia mbegu zake za kiume kwenye benki hiyo.
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo anayechezea timu ya Real Madrid ya Hispania naye yumo kwenye listi hiyo ya masupastaa na mbegu zake za kiume zinahitajika kwa euro milioni 50.
Cryobank kwa miaka 30 sasa imekuwa ikijishughulisha na upandikizaji wa mimba kwa wanawake kwa kutumia mbegu za kiume za watu wanaojitolea kwenye benki hiyo.
Cryobank imekuwa ikijiingizia mamilioni ya dola kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaotaka kupata watoto kwa njia ya upandikizaji wa mbegu za kiume.
taarifa zaidi....... www.nifahamishe.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment