Thursday, June 12, 2008

WACHAGA NI BALAA

Huku ndo kwenyewe Uchagani!!!!


Familia moja ilishangazwa pale walipopokea jeneza la marehemu mama yaoaliyefariki nchini Marekani.. Lilitumwa na mmoja ya watoto wake wa kike.Mwili ndani ya jeneza ulikuwa umesongwa sana ndani ya jeneza kiasikwamba uso wa marehemu ulikuwa umegusa kioo cha jeneza!Walipofungua jeneza, walikuta barua juu ya merehemu, iliyosomeka namnahii:"Wapendwa ndugu zangu, nimeutuma mwili wa mama yetu kwa ajili yamazishi, kwani imekuwa siku zote hamu yake kubwa kuzikwa nyumbani Machame, katika nyumba ya ukoo. Samahani sikuweza kuja na mwili kwaninimenyimwa likizo kwani kuna upungufu wa wafanyakazi hapa kazini mwezihuu.Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa mama, kuna makopo 12 ya samaki wamakopo, paketi 10 za supu ya Royco na chupa 8 za jam ya maembe. Mgawanehivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi.Katika miguu ya mama kuna pea moja ya viatu vya Reebok namba 9 kwa ajiliya mtoto mkubwa wa Mushi. Pia, kuna pea mbili za viatu kwa ajili yawatoto wa Urassa na Kwayu, natumaini nitakuwa sijakosea namba za miguu.Nimemvalisha pia mama American T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili yaManka, na zinazobaki ni za watoto wake. Hizo jeans mpya 2 ambazo mamaamezivaa ni za wavulana Elirehema na Munnisi. Hiyo Swiss watch mkono wake wa kushoto nizawadi ya Verynice kwa ajili ya sikukuu yake ya kutimiza miaka 21. AntiRebeka, hizo heleni, mkufu na pete ambazo mama amevaa ni zako.Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa wagaiwe wajomba. Tafadhali mgawane kamanilivyosema na kama kuna kitu kingine mnahitaji, basi mnieleze kwanihali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana.Dada yenu mpenzi,Mama Manka


Wachaga mmezidi…….Vya hivi hamna……….!!!!!!???

No comments: