Sunday, November 8, 2009
JEURI ya PESA
Bilionea mmiliki wa timu ya Chelsea ya Uingereza Roman Abramovich alitumbua dola 52,000 (Takribani Tsh. 68,000) kwaajili ya chakula chake cha mchana pamoja na marafiki zake tisa kwenye mgahawa mmoja maarufu wa jijini New York nchini Marekani.
Abramovich mwenye umri wa miaka 42 alitumia jumla ya dola 47,221 kwaajili ya msosi wake na marafiki zake tisa akiwemo mpenzi wake Dasha Zhukova na mtoto wake wa kiume Arkady.
Baada ya chakula hicho Abramovich alitoa bakshishi ya dola 5,000 kwa wahudumu wa mgahawa Nello's restaurant uliopo kwenye mtaa maarufu wa Madison Avenue.
Pesa alizotumia Abramovich kwenye mgahawa huo ni nyingi sana kulinganisha na nyota wa Hip Hop, Jay-Z, ambaye alitumbua dola 1,000 kwenye mgahawa huo huo wiki iliyopita.
Asilimia kubwa ya pesa alizotumbua kwenye mgahawa huo zilitokana na shampeni za kifahari alizonunua.
Abramovich alinunua chupa mbili za shampeni ya Chateau Petrus zilizogharimu dola 10,000 na chupa tatu za shampeni ya kiitaliano ya La Tache Romanee Conti zilizogharimu dola 15,000.
Mmoja wa watu walioshuhudia risiti ya malipo ya Abramovich alishangazwa sana na kiasi hicho kikubwa cha pesa lakini alisema kwamba kwa pesa walizonazo matajiri kama Abramovich ni sawa na kama vile amenunua chupa moja ya bia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment