
Nauli mpya za daladala na mabasi ya mikoani zinaanza kutumika nchi nzima kesho huku wananchi wakiwa na hofu ya nauli hizo kupandishwa zaidi ya ilivyotangazwa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).
Wasiwasi huo umetokana na nauli nyingi zilizotangazwa kupanda kuwa tayari zimeanza kutumika kabla ya Sumatra kutangaza nauli mpya.Akizungumza Dar es Salaam Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray alisema mamlaka hiyo imejipanga vizuri kuhakikisha nauli mpya zinatumika kama ilivyokusudia ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti makondakta wanaotoza nauli zaidi.Katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo, mabasi yaendayo Arusha na Kilimanjaro yaliendelea kukata nauli ya zamani kwa ajili ya safari za kesho wakisema kuwa kwa sasa abiria ni wachache waendao mikoani.
Mmoja wa makarani wa mabasi yaendayo Arusha na Dodoma ya Happy Nation, Seleman Majati alisema nauli mpya inaweza kutumika katika kipindi cha Sikukuu hasa Desemba lakini kwa sasa ni maelewano kati ya abiria na makarani hao kutokana na uchache wa abiria.
zaidi....http://lukwangule.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment